Nani anatafuta mwenzake zaidi? Sasa unaweza kujua
Sote tuna marafiki tunaoongea nao kila siku, halafu kuna wale tunaodhani tuliongea nao “juzi tu” hadi watukumbushe kwamba kumbe ni mwezi mzima umepita.
Kudumisha mawasiliano kunahitaji juhudi kutoka pande zote mbili, lakini si kila mtu anakumbuka mambo kwa namna moja. Mmoja ana uhakika kwamba yeye ndiye hupiga simu kwanza kila mara. Mwingine naye anaapa kwamba hupiga mara nyingi tu. Mwishowe, mara nyingi ni hisia tu.
Kwa hiyo badala ya kubishana, sasa unaweza kuangalia tu.
Ukiwa na Me, unaweza kuona takwimu za kuvutia kuhusu uhusiano wako na anwani fulani moja kwa moja kwenye wasifu wake. Si tu nani amemhifadhi nani, bali pia mmeongea kiasi gani, mmepigiana simu mara ngapi na mnashiriki taarifa zipi.
Unaona nini kwenye wasifu?
Ukifungua wasifu wa anwani kwenye Me, unaweza kugundua mambo kama:
Mna anwani za pamoja ngapi, na ni akina nani
Amekuhifadhi kwa jina gani kwenye anwani zake
Wewe umemhifadhi kwa jina gani kwenye anwani zako
Umbali kati yenu, kama nyote wawili mmekubali kushiriki umbali
Mmepigiana simu mara ngapi
Mmeongea kwa muda gani kwa jumla
Taarifa hizi zinakupa mtazamo mdogo lakini wa kuvutia kuhusu uhusiano wenu, na wakati mwingine hata kujibu lile swali kubwa: nani kweli anatafuta mwenzake?
Kwa hiyo, nani alipiga zaidi?
Tuseme Wanjiku, rafiki yako wa karibu tangu darasa la kwanza, anakuambia kwamba yeye tu ndiye hupiga simu. Kwake, yeye ndiye hujitahidi kila wakati.
Wewe, kwa upande wako, una uhakika si kweli. Unaapa ulimpigia mara kadhaa wiki hii tu.
Badala ya kujaribu kukumbuka nani yuko sahihi, fungua tu wasifu wa Wanjiku kwenye Me na uangalie takwimu.
Mmepigiana simu mara ngapi.
Mmeongea kwa muda gani.
Na nani alimpigia mwenzake zaidi.
Wakati mwingine utagundua Wanjiku alikuwa sahihi. Wakati mwingine utagundua ni wewe. Vyovyote vile, huenda mkapata cha kucheka.
Mnadhani mko karibu? Gundueni na mshiriki!
Ndani ya wasifu utakuta pia kitufe kipya:
“Think you're close? Find out & share!” (Mnadhani mko karibu? Jua na ushiriki!)
Kiguse, na skrini maridadi ya kushiriki itafunguka, ikionyesha takwimu za uhusiano wenu kwa njia wazi na ya kuvutia. Skrini hiyo inajumuisha maelezo kama kila mmoja wenu amepiga simu mara ngapi, jumla ya muda wa simu na ulinganisho kati yenu wawili.
Unaweza kushiriki skrini hii na marafiki, kwenye magroup au kwenye mitandao ya kijamii kwa kugusa mara moja tu.
Kwa hiyo ukigundua umepotea kidogo siku za karibuni, labda ni wakati wa kuchukua simu na kupiga. Na kama takwimu zinaonyesha wewe ndiye unayedumisha mawasiliano, shiriki skrini na uache ukweli ujisemee wenyewe
Unaipataje?
Fungua programu ya Me
Nenda kwenye wasifu wa anwani unayoitaka
Angalia taarifa mnazoshiriki

Gusa “Think you're close? Find out & share!”
Shiriki skrini kwa kugusa mara moja
Ukiwa na Me, hata urafiki wako unapata hadithi yake ndogo.
