Muhtasari wa Simu. Tunaishi katika dunia inayokwenda kwa kasi.
Kila mtu ana shughuli, ana haraka, muda haumtoshi. Tuna mipango, kazi za kukamilisha, mahusiano ya kudumisha na mambo ya kufanya
Skrini ya muhtasari wa simu itakusaidia kukamilisha baadhi ya vitendo kwa mafanikio na kwa muda mfupi.
(Android pekee)
Simu ikiisha, skrini yetu mpya ya “Call Summary” (Muhtasari wa Simu) itajitokeza yenyewe, na chaguo zote unazohitaji zitaonekana ili usipoteze muda. Kwa kugusa mara moja unaweza kushiriki maelezo yako na kutuma ujumbe wa WhatsApp ndani ya sekunde chache.
( huhitaji kamwe kusave namba ili kutuma WhatsApp)
Skrini ya muhtasari wa simu inakuwezesha kufanya vitendo vingi haraka na kwa ufanisi, na kila kitu kiko kiganjani mwako. Kwa mfano:
yote kwa kugusa mara moja!
1. Tuma ujumbe wa WhatsApp.
2. Ongeza namba kwenye anwani.
3. Tuma SMS.
4. Piga tena.
5. Shiriki maelezo yako binafsi.
6. Zuia namba.
7. Shiriki taarifa za anwani.
8. Mtumie mtumiaji barua pepe.
9. Ongeza namba kwenye vipendwa.
10. Tazama takwimu za simu kati yako na anwani hiyo
* (ikiwa tu namba imehifadhiwa kwenye anwani zako).
11. Muda wa simu.
12. Shiriki anwani.
Unaweza pia kupitia simu za karibuni kwa urahisi kwa kutumia mishale na kuruka kutoka simu moja hadi nyingine,
na ukigusa picha ya aliyepiga, programu itakuonyesha wasifu wake kamili na maelezo zaidi.
Kama umeshiriki mahali ulipo na anwani hiyo, utaweza kuona mahali hapo kwenye skrini.

Unahitaji kupiga namba ileile tena na ungependa kukumbushwa?
Hakuna shida! Sisi wa Me tutakukumbusha. Ukigusa lebo, skrini itafunguka ikiwa na chaguo tatu za muda wa kikumbusho:
- Baada ya saa moja kuanzia sasa.
- Baada ya saa mbili kuanzia sasa.
- Kesho saa ileile.
Na kama unataka kuandika dokezo la faragha, hilo pia linawezekana. Tunajua una shughuli nyingi na hatutaki usahau.
Tafadhali kumbuka:
Skrini ya muhtasari wa simu ikifunguka, ukigusa popote kwenye skrini itafungwa
Kama hupendi kipengele hiki, unaweza kuzima skrini hii kwa urahisi:
→ Ingia kwenye mipangilio ya programu → Chagua Call Summary (Muhtasari wa Simu) → na uzime swichi!
* Ukishaizima, skrini haitajitokeza tena simu ikiisha. *

