Zuia namba kwa urahisi kabisa.. acha kupokea simu/SMS! kutoka namba usizozitaka
Me ina mfumo mpya wa kuzuia
Kipengele hiki ni bure na kinafanya kazi kwenye vifaa vya iOS na Android!
Kama ukimya ni dhahabu, kublock ni dhahabu tupu
Umeishi maisha yako yote bila kumblock mtu yeyote?
Hongera: ama wewe ndiye mtu mwenye bahati zaidi duniani, ama bado HUJAKUTANA na watu wasioelewa maana ya mipaka, wanaopenda kutumia simu zao kutusumbua sisi wengine maskini.
Kama sivyo, basi wewe ni chuma, na una subira ya ajabu.
Mungu akubariki.
Vyovyote vile, wengi wetu tumewahi kujikuta kwenye hali halisi ambapo ilitubidi kuwazuia watu/ wasiwasiliane nasi.
Lakini linapokuja suala la mawasiliano ya simu, tuko hapa kukupa suluhisho kwa changamoto yoyote,
iwe ni kutambua anayepiga, kuzuia simu za spam na utapeli, na vipengele vingine vingi vilivyoundwa kwa urahisi wako.
Tumeongeza chaguo mbili mpya za kuzuia kwenye caller ID
ili uzuie kwa urahisi namba za simu za watu ambao hutaki kuwasiliana nao wakati wowote ule.
Bado huna Me? Pakua sasa

Jinsi ya kuzuia au kuondoa kizuizi cha namba / mtumiaji wa Me:
Kama unataka kuzuia mtu aliye kwenye anwani zako au hata namba yoyote ile, fanya hivi: fungua programu ya Me
gusa wasifu wa anwani/namba hiyo ili kufungua → wasifu wa Me,
shuka chini, kisha uguse "Block Number" (Zuia namba).
Baada ya hapo, dirisha litafunguka lenye chaguo mbili za kuzuia:
- Block number (Zuia namba) - Namba hiyo haitaweza kukutumia SMS wala kukupigia simu.
- Block Me profile (Zuia wasifu wa Me) - Mtumiaji huyo hataweza kuona wasifu wako, na wewe hutaona wake.
Umeamua kumpa mtu nafasi nyingine maishani mwako, na unataka kumuondolea kizuizi?
Gusa nembo ya Me-> Settings->Gusa Blocking Settings (Mipangilio ya kuzuia)-> Chagua namba
"Unblock Number" (Ondoa kizuizi). Au badilisha kizuizi chako kwa kutelezesha kushoto
Jinsi ya kuzuia namba / mtumiaji wa Me simu ikishakatika kupitia muhtasari wa simu (Android pekee)
Tunatumaini tumekusaidia
